Umoja wa Ulaya wahimiza diplomasia mzozo wa Hormuz
17 Machi 2026
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas amesema Umoja wa Ulaya unataka njia za kidiplomasia zitumike kutafuta mwafaka wa kuufungua mlango bahari wa Hormuz.
Kauli hiyo imetolewa baada ya miito ya rais Donald Trump wa Marekani ya kuwataka washirika wake wapeleke meli za kivita kwenye eneo hilo kutowa ulinzi kufuatia vita dhidi ya Iran.
Washirika wa Marekani wakataa ombi la Trump la kupeleka Meli zao Hormuz
Kallas ameweka wazi kwamba hakuna anayetaka kuhatarisha maisha ya watu wake katika mlango bahari wa Hormuz na kwa hivyo kuepusha mgogoro wa chakula, mbolea na nishati, njia za kidiplomasia zinapaswa kutumika kuutatua mgogoro huo.
Rais Trump ameyatishia mataifa ya jumuiya ya NATO kwamba mustakabali wao utakuwa mbaya ikiwa yatakataa kupeleka meli za kijeshi kwenye mlango bahari wa Hormuz.Hezbollah
Ujerumani na mataifa kadhaa ikiwemo Japan, Poland,Uhispania, Sweden na Australia yamekataa wito wa Trump.