1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wathibitisha kurejesha vikwazo dhidi ya Iran

29 Septemba 2025

Umoja wa Ulaya umethibitisha leo kuwa umerejesha vikwazo dhidi ya Iran, kufuatia hatua kama hiyo iliyochukuliwa na Umoja Mataifa.

Ufaransa Straßburg | bunge la Umoja wa Ulaya
Bunge la Umoja wa UlayaPicha: Yves Herman/REUTERS

Katika taarifa, urais wa Umoja huo umesema kuwa umechukuwa hatua hiyo kwa kujibu hatu ya Iran ya kutozingatia makubaliano ya nyuklia. Hata hivyo umesema milango ya mazungumzo ya kidiplomasia bado iko wazi.

Umoja huo umesema vikwazo hivyo vinajumuisha kufungia mali ya benki Kuu ya Iran na nyingine za nchi hiyo pamoja na marufuku za usafiri dhidi ya baadhi ya maafisa wa Iran.

Raia wa Irana walalamika kuhusu vikwazo

Hatua hiyo imepokelewa kwa maoni mseto nchini Iran.

Nasim Company, mtafiti wa nchi za Asia ya Kusini na Afghanistan amesema kuwa wataharibikiwa.

Ameongeza kuwa vikwazo hivyo vitachangia kuzuka kwa matatizo mengine makubwa katika jamii.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW