1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGeorgia

Umoja wa Ulaya watishia kuiwekea Georgia vikwazo

11 Desemba 2024

Umoja wa Ulaya unatishia kuiwekea vikwazo Georgia kufuatia matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji.

Maandamano Tbilisi | Georgia
Georgia yashutumiwa kutumia nguvu zaidi dhidi ya waandamanaji wanaoegemea upande wa Umoja wa Ulaya.Picha: Pavel Bednyakov/APpicture alliance/dpa

Umoja wa Ulaya umetishia kuiwekea vikwazo serikali ya Georgia kufuatia machafuko na matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji wanaoegemea upande wa Umoja huo wa Ulaya.

Msemaji wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas amesema hatua zinazoweza kuchukuliwa zitajadiliwa katika mkutano wa mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja huo Jumatatu wiki ijayo.

Hata hivyo hakuweka wazi ni vikwazo vya aina gani vitakavyojadiliwa kwenye mkutano huo lakini pia amesema matumizi ya nguvu sio suluhisho la kuzima maandamano ya watu wanaodai kuona demokrasia na mustakabali wa Georgia katika Umoja wa Ulaya.

Hata hivyo Hungary imeshatishia kwamba itapinga hatua yoyote ya kupitishwa vikwazo dhidi ya Georgia.

Maandamano ya Georgia yamechochewa na uchaguzi wa bunge uliofanyika hivi karibuni,wanaodai ulikumbwa na dosari nyingi, na hatua ya chama tawala ya kutangaza kusitisha mazungumzo ya kutaka kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya, hadi mwaka 2028.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW