1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaUbelgiji

Umoja wa Ulaya watoa mkopo usio na riba kuisaidia Ukraine

19 Desemba 2025

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kutoa mkopo usiokuwa na riba wa euro bilioni 90 kwa Ukraine ili kusaidia mahitaji yake ya kijeshi na kiuchumi katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Ubelgiji | Brüssel 2025 | Friedrich Merz | Umoja wa Ulaya EU
Kansela wa Ujerumani Friedrich MerzPicha: John Thys/AFP/Getty Images

Viongozi wa EU hata hivyo bado hawajafikia mwafaka na Ubelgiji kuhusu pendekezo la kutumia mali za Urusi zilizozuiwa ndani ya Umoja huo kama chanzo cha kukusanya fedha za mkopo huo.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amesema makubaliano hayo ni hatua muhimu mbele, akibainisha kuwa kukopa kupitia masoko ya mitaji ndio chanzo halisi na kinachowezekana zaidi kwa wakati huu ili kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.

Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz, pia amepongeza uamuzi huo wa viongozi wa Umoja wa Ulaya wa kuipatia Ukraine mkopo usio na riba.

"Ulaya imeupokea ujumbe. Ulaya imeonyesha uwezo na mamlaka yake. Tunasimama imara dhidi ya tishio kubwa zaidi kwa usalama barani Ulaya — uchokozi wa Urusi ambao kwa muda mrefu umevuka mipaka zaidi ya uvamizi dhidi ya Ukraine," amesema Merz.

Baada ya takriban miaka minne ya vita, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) linakadiria kuwa Ukraine itahitaji euro bilioni 137 katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW