Umoja wa Ulaya watoa msaada wa fedha kwa Afrika
18 Julai 2008Matangazo
Lengo la hatua hiyo ni kuliwezesha bara hilo kukimu mahitaji yake ya chakula.Ahadi hiyo ilitolewa hapo jana jioni mjini Dar es Salaam nchini Tanzania wakati wa kikao cha siku mbili kinachojadilia ushirikiano wa kikanda kati ya eneo la Afrika mashariki na Kusini vilevile eneo la bahari ya Hindi.
Mwandishi wetu wa Dar es Salaam Pascal Mayala alihudhuria kikao hicho na kuandaa taarifa ifuatayo.