1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umwagaji damu waendelea Syria

Mnette,Sudi/rtre,afp8 Mei 2011

Watu sita waliuawa hapo jana nchini Syria, baada ya vikosi vya serikali kushambulia bandari ya Banias kaskazini mwa nchi.

Waandamanaji katika mji wa Banias
Waandamanaji katika mji wa BaniasPicha: dapd

Wanaharakati nchini humo wamesema, miongoni mwa watu waliouawa ni waandamanaji wanne wa kike waliokuwa wakigombea kuachiliwa huru kwa watu waliokamatwa.

Ripoti zimesema kuwa idadi kadhaa ya vifaru na magari ya kijeshi yameingia mji huo wa kaskazini-magharibi.

Makundi ya haki za binaadamu yanasema takriban watu 26 waliuawa siku ya Ijumaa katika maandamano yaliyofanywa kote nchini kuishinikiza serikali ya mabavu ya Rais Bashar al-Assad wa Syria kuondoka madarakani.

Umoja wa Ulaya umeweka vikwazo vya silaha dhidi ya Syria na marufuku ya kusafiri dhidi ya maafisa 13 wa serikali hiyo na mali yao pia imezuiliwa. Marekani nayo imetishia kuchukua hatua mpya dhidi ya kile kilichoitwa "vitendo vya kusikitisha" vinavyofanywa na serikali ya Syria.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi

Onesha taarifa zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW