1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Afghanistan ni taifa kandamizi zaidi duniani

9 Machi 2023

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan umesema kuwa viongozi wapya wa nchi hiyo wameonesha lengo moja la kuweka sheria ambazo zinawaacha wanawake na wasichana wengi wakiwa wamekwama majumbani mwao.

Katar Taliban Friedensgespräche
Picha: Ibraheem al Omari/REUTERS

Katika tathmini yake wakati wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake hapo jana, umoja huo ulisema tangu uongozi wa Taliban uingie madarakani mnamo Agosti mwaka 2021, taifa hilo limekuwa kandamizi zaidi duniani kwa wanawake na wasichana, kwa kuwanyima haki zao zote za kimsingi.

UN. yaonya dhidi ya ukandamizaji wa wanawake Afghanistan

Mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja huo wa Mataifa Roza Otunbayeva ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa kisiasa wa Umoja huo nchini Afghanistan, ameliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York kwamba viongozi wa Taliban wanadai kuwa wameliunganisha taifa hilo lakini pia wameligawanya vibaya katika misingi ya kijinsia.