1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

UN yaonya juu ya amri za Israel kutaka Wapalestina kuhama

23 Agosti 2024

Umoja wa Mataifa umeonya juu ya amri za jeshi la Israel za kuwataka watu wahame kutoka kwenye maeneo mbalimbali katika Ukanda wa Gaza kuwa zinahatarisha maisha ya raia badala ya kuwalinda.

Wakaazi wa Gaza wakiondoka baada ya kuagizwa na Israel
Watu wakikimbia kutoka eneo la mashariki mwa Gaza baada ya mamlaka za Israel kuwaagiza kuondoka Picha: Rizek Abdeljawad/Xinhua/IMAGO

Hayo yamesema na afisa wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu katika eneo la Palestina, Muhannad Hadi.

Hadi, amesema maagizo hayo ya jeshi la Israel yamewafanya asilimia 90 ya wakaazi wa Gaza milioni 2.1 kuwa wakimbizi wa ndani tangu vita vya Israel na Hamas vilipoanza.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu imesema wajumbe kutoka nchi hiyo wamewasili Cairo kuanza tena juhudi za kufukia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Wakati huo huo, mapigano yanaendelea katikati mwa Ukanda wa Gaza leo Ijumaa, licha ya wapatanishi wa Marekani, Qatar na Misri wakiendelea na mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza.