JamiiUswisi
Idadi ya watoto wanaochomwa chanjo yaongezeka
18 Julai 2023Matangazo
Mkuu wa chanjo katika Shirika la Afya Duniani WHO Kate O'Brien, lakini, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa bado kuna mapungufu makubwa yaliyo na hatari.
Mkuu wa WHO asema takwimu zilizotolewa zinatia moyo
Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebrayesus amekubaliana na hayo na kusema takwimu hizo zilizotolewa zinatia moyo. Ghebreyesus lakini ameonya kwamba wastani wa takwimu za dunia na kikanda hazitoi picha kamili na zinafunika tofauti za usawa zilizopo.
Licha ya takwimu hizo, watoto milioni 20.5 walikosa kuchomwa chanjo moja au zaidi za kawaida mwaka 2022.