UN: Dola bilioni 1 zahitajika kusaidia waathirika wa Uturuki
17 Februari 2023Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kukusanywa kiasi cha dola bilioni moja kushughulikia mzozo wa kibinadamu unaozidi kuongezeka nchini Uturuki na Syria baada ya tetemeko la ardhi la Februari 6. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema katika taarifa yake kwamba fedha hizo zitatoa misaada ya kibinadamu kwa miezi mitatu kwa watu milioni 5.2. Siku 11 baada ya tetemeko hilo, waokoaji wa Uturuki walifanikiwa jana kumwokoa msichana wa miaka 17 na mwanamke mwenye umri wa miaka 20 kutoka kwenye vifusi lakini matumaini ya kuwapata manusura wengine yanaendelea kufifia. Hadi sasa watu 41,000 wamethibitishwa kuuawa na tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa 7.8 katika kipimo cha Richter, ambalo limeorodheshwa kuwa mojawapo ya matukio 10 mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 100 iliyopita.