1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Hali ya vita vya Tigray inazidi kuwa mbaya zaidi

19 Oktoba 2022

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kwamba hali ya vita katika jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray inazidi kuwa mbaya na idadi ya raia wanaouwawa inaongezeka wakati jeshi likitangaza kunyakua miji mitatu.

Äthiopien Tigray Shire | eritreisches Flüchtlingslager
Picha: Joerg Boethling/IMAGO

Serikali ya Ethiopia ilitowa taarifa jana ikisema jeshi lake la ulinzi limechukua udhibiti wa miji ya Shire,Alamata na Korem bila ya makabiliano katika maeneo hayo ya mijini. Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikitowa miito ya vita kusitishwa katika jimbo hilo la Tigray tangu ziliposhindwa juhudi za Umoja wa Afrika mwanzoni mwa mwezi huu za kuzileta pamoja pande zonazohasimiana kwenye meza ya mazungumzo. Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kupitia msemaji wake Ravina Shamdasani  inasema hali ni mbaya na raia wanaendelea kuuwawa.Guterress: Hali inaendelea kuwa mbaya Ethiopia

''Hali ya hivi sasa ya mashambulizi ya anga ya kushtuwa katika jimbo la Tigray inahatarisha sana kuongezeka kwa athari za vita dhidi ya raia''

Kinachotokea hivi sasa katika jimbo hilo la Tigray ni mapigano mapya katika mgogoro wa vita vya miaka miwili vinavyoendeshwa na vikosi vya serikali ya Ethiopia na washirika wao dhidi ya wapiganaji wa chama cha ukombozi wa watu wa Tigray TPLF.

Wanajeshi wa Ethiopia Picha: AMANUEL SILESHI/AFP/Getty Images

Kabla ya tangazo la serikali ya waziri mkuu Abiy Ahmed kutolewa kuhusu kudhitiwa kwa miji hiyo mitatu,kamandi kuu ya Tigray ilitangaza kwamba mji wa kimkakati wa Shire na maeneo mengine yameangukia mikononi mwa vikosi vya uvamizi.

Aidha katika ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na haki za binadamu,akitowa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na hali ya Tigray,msemaji wa ofisi hiyo Ravina Shamdasani alisema tangu Agosti 31 wamepokea ripoti kadhaa za kuuwawa raia na uharibifu wa mali za raia kufuatia mashambulizi ya anga pamoja na mashambulizi ya makombora katika jimbo la Tigray na kutokana na hali ya mawasiliano kuwa mbaya ni ni vigumu sana kuthibitisha kuhusu ripoti hizo ingawa ni wazi kwamba idadi ya raia waliouwawa imekuwa ikiongezeka.Muungano wa Afrika waandaa mazungumzo ya amani Ethiopia

Shamdasani amekosoa mashambulizi yanayowalenga raia kwa kuweka wazi kwamba haikubaliki katika sheria ya kimataifa.

"Chini ya sheria ya kimataifa,mashambulizi yakiholela,yasiyoweka mipaka au mashambulizi yanayowalenga kwa makusudi raia au maeneo ya raia ni jambo linaweza kuwa  uhalifu wa kivita''

Mapigano mapya kati ya vikosi vya serikali na TPLF yalianza tangu mwishoni mwa Agosti wakati pande zote mbili kila mmoja akimtupia mwenzake lawama ya kuwa chanzo cha kuvunja makubaliano ya miezi mitano ya kusitisha vita,makubaliano ambayo yalitowa fursa ya kupelekwa kwa muda msaada wa kibinadamu katiba jimbo la Tigray na kutowa alau matumaini.

  

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW