1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Jamhuri ya Afrika ya Kati yaathirika na mzozo wa Sudan

Hawa Bihoga
15 Juni 2024

Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa umeonesha kuwa vikosi vya kijeshi vya Sudan vinalitumia taifa la Jamhuri ya Afrika ya Kati kama "Mnyororo wa ugavi" ikiwa ni pamoja na kuajiri wapiganaji.

Umoja wa Mataifa | Baraza la Usalama katika vikao vyake.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika vikao vyake.Picha: Eduardo Munoz/REUTERS

Katika ripoti iliotolewa na kamati ya wataalamu ilioundwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ilioonesha wasiwasi kuhusu "athari za ziada" katika mzozo huo inasema kwamba, Jamhuri ya Afrika ya Kati imeathirika pakubwa na mzozo unaoendelea Sudan.

Ripoti ya kamati hiyo iliangalia masuala kadhaa ikiwemo hali ya kiutu wakati taifa hilo likishuhudia wimbi la mamilioni ya wakimbizi kutoka Sudan, uvamizi wa pande mbili zinazohasimiana pamoja na uvamizi wa anga wa jeshi la Sudan karibu na kituo cha mpakani cha Umm Dafog ambapo ni kitovu cha wanamgambo wa RSF.

Soma pia:Marekani yaongeza msaada kwa Sudan kupambana na njaa

Aidha wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa wameitolea mwito serikali ya Afrika ya Kati kukabiliana na ongezeko la biashara haramu ya silaha kutoka mataifa jirani ikizingatiwa hali ilivyo kwa sasa nchini Sudan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW