1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Kipindi cha mpito cha Syria bado ni tete

7 Desemba 2025

Jopo la wachunguzi wa Umoja wa Mataifa limesema leo kuwa kipindi cha mpito cha Syria bado ni tete, mwaka mmoja baada ya kupinduliwa kwa Bashar al-Assad, na kwamba hali ya kulipiza kisasi inapaswa kukomeshwa.

Syria Damascus 2025 | Ahmad al-Sharaa
Rais wa mpito wa Syria Ahmad al-Sharaa akiwa Damascus mnamo Januari 10, 2025Picha: Giuseppe Lami/ANSA/picture alliance

Jopo hilo liliipongeza Syria kwa hatua ambayo imechukua hadi sasa kushughulikia uhalifu na unyanyasaji uliotekelezwa katika miongo iliyopita.

Lakini limesema matukio ya ghasia tangu kuanguka kwa utawala wa Assad yamesababisha watu kukimbia tena makazi yao na mgawanyiko, hali inayoibua wasiwasi juu ya mwelekeo wa baadaye wa nchi hiyo.

Jopo hilo la Umoja wa Mataifa limesema "orodha ya kutisha" ya unyanyasaji uliofanywa na serikali ya Assad "ni sawa na ghasia za uhalifu wa kiviwanda" dhidi ya watu wa Syria.

Jopo hilo la watu watatu lina jukumu la kubaini ukweli kwa nia ya kuhakikisha kwamba wahusika wa ukiukaji huo hatimaye wanawajibishwa.