1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

UN: Korea Kaskazini yazidisha ukandamizaji, watu wafa njaa

18 Agosti 2023

Korea Kaskazini inaelezwa kuzidisha ukandamizaji wake wa haki za binadamu na raia wa taifa hilo wanazidi kukata tamaa.

Volker Turk, mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa akitoa hotuba kwenye kikao mkutano wa 53 wa haki za binadamu mjini Geneva Uswisi.
Volker Turk, mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa akitoa hotuba kwenye kikao mkutano wa 53 wa haki za binadamu mjini Geneva Uswisi.Picha: Pierre Albouy/KEYSTONE/picture alliance

Kuna pia ripoti za watu kufa kwa njaa katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo, huku hali ya uchumi ikizidi kuwa mbaya.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa ofisi ya Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk katika mkutano wa kwanza wa haki za binaadamu kuhusu Korea Kaskazini tangu mwaka 2017.

Kiongozi huyo wa ofisi ya Umoja wa Mataifa amesema taarifa walizonazo ni kwamba watu wamekuwa na hofu ya kufuatiliwa na serikali, kukamatwa, kuhojiwa na kuwekwa kizuizini.

Kama mifano ya kuongezeka kwa ukandamizaji wa haki za binadamu, alisema, mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kufuatilia habari za itikadi za kigeni na haswa kutoka Korea Kusini inawezekana akafungwa miaka 5 hadi 15 gerezani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW