UN kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu Belarus
19 Mei 2021Matangazo
Bachelet amemteua Karinna Moskalenko ambaye ni wakili wa haki za binadamu kutoka Urusi na ambaye atahudumu kama mwenyekiti. Mwengine aliyeteuliwa ni Susan Bazili ambaye ni wakili wa haki za binadamu kutoka Canada na Marko Milanovic ambaye ni profesa wa sheria kutoka Serbia.
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko ambaye ameiongoza nchi hiyo kutoka mwaka 1994 alishinda muhula wa sita katika uchaguzi huo uliofanyika mwezi Agosti mwaka jana na ambao upinzani na wanadiplomasia wa nchi za Magharibi wanasema ulikumbwa na udanganyifu.
Alikabiliwa na maandamano ambapo maelfu ya waandamanaji walikamatwa na zaidi ya mia nne kupewa vifungo vya muda mrefu jela.