1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN kufanya mkutano kuhusu teknolojia ya akili bandia.

17 Julai 2023

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litafanya mjadala wake wa kwanza kuhusu teknolojia ya akili bandia wiki hii mjini New York huku Uingereza ikitarajiwa kutoa wito wa mdahalo wa kimataifa.

USA UN-Sicherheitsrat
Picha: Loey Felipe/UN Photo/Xinhua/IMAGO

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza James Cleverly ataongoza majadiliano hayo ya kesho Jumanne.

Serikali kote ulimwenguni zinafikiria jinsi ya kupunguza athari za teknolojia ya akili bandia inayojitokeza, ambayo inaweza kubadilisha uchumi wa dunia na mazingira ya usalama wa kimataifa.

Soma pia:Jinsi gani serikali zitadhibiti teknolojia ya akili bandia?

Mnamo mwezi Juni, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, aliunga mkono pendekezo lililotolewa na baadhi ya maafisa wakuu wa teknolojia ya akili bandia.

Pendekezo hilo lilihusu kuundwa kwa shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi yake kama vile Shirika la Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa, IAEA.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW