UN: Kuna ongezeko la unene kupindukia kwa watoto na vijana
10 Septemba 2025
Umoja wa Mataifa umetahadharisha juu ya tatizo la watu kunenepa kupindukia ambalo limeongezeka maradufu miongoni mwa watoto na vijana. Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limesema matumizi ya vyakula vinavyotengenezwa viwandani na matangazo ya vyakula visivyofaa kiafya yamelifanya tatizo hilo kuongezeka mno.
UNICEF imeonya kwamba kwa sasa tatizo hilo limeongezeka zaidi miongoni mwa watoto wa umri wa miaka mitano hadi vijana wa miaka 19 na kwa sasa limepita hata tatizo la utapiamlo.
Ripoti ya UNICEF imefafanua kwamba kama ambavyo ilitarajiwa awali kwamba hadi mwisho wa mwaka huu wa 2025 mtu mmoja katika kundi hilo la la watu atakuwa na tatizo la kunenepa kupita kiasi.
Mkuu wa shirika la UNICEF Catherin Rusell amesema kwamba maana ya neno utapiamlo sasa linabadilika kutokana na tatizo hilo.
"Leo tunapozungumzia utapiamlo hatumaanishi ukosefu wa lishe bora wala kukonda kupita kiasi."
Katika ripoti yenye kutia wasiwasi kutoka shirika la UNICEF vyakula vya viwandani vinaendelea kuchukua nafasi ya matumizi ya matunda,mboga na protini katika kipindi ambacho mtoto anahitaji aina hii ya vyakula katika makuzi yake.
Ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, sukari na chumvi
Shirika hilo linasema kwamba jambo la kutisha ni kwamba kwa hali hii mtu 1 kati ya 10 walioko kwenye kundi hilo la umri wa miaka 5 hadi 19 anakabiliwa na magonjwa sugu yanayosababishwa na urahisi wa kupata vyakula hivi vya viwandani.
Kwa upande mwingine UNICE imesema kwamba juhudi za kupambana na njaa kote duniani hadi sasa zimezaa matunda kwa sababu tatizo la kupoteza uzito limepungua kutoka asilimia 13 hadi asilimia 10 kati ya mwaka 2000 na 2022. Huu ni utafiti uliofanywa katika nchi 190 zikiwemo zile zilizoendelea na zinazoendelea kiasi kwamba idadi ya waathirika ilizidi mara mbili kutoka watu 194 mwaka 2000 hadi watu 391 mwaka 2022.
Katika hali ambayo haikutegemewa kiasi cha watu wenye tatizo la unene wa kupindukia kwa mara ya kwanza limepanda kwa asilimia 9.4% zaidi ya watu wenye tatizo la kukonda kupita kiasi chini ya kiwango katika asilimia 9,2%.
Kulingana na makadirio ya ripoti ya UNICEF watu milioni 188 wakiwemo watoto na vijana kote ulimweguni wana tatizo la uzito wa kupindukia.
Unene kupindukia umeenea katika familia za kipato cha juu
Shirika la UNICEF limesema kwamba matatizo haya hayasababishwi na ukosefu wa lishe bora miongoni mwa familia maskini na tajiri isipokuwa linasababishwa na mienendo isiyofuata misingi bora ya matumizi ya vyakula.
Watafiti wamesema kwamba hali hii haisababishwi na watoto hao au familia zao isipokuwa mazingira duni ambamo watu wanashindwa kutunza mazingira yao.
Kwa kawaida kiwango cha unene wa kupindukia kimekuwa kikiripotiwa katika nchi zilizoendelea hasa katika nchi kama Chile ambapo asilimia 27% ya watu walio kwenye kundi hilo la watu umri wa miaka 5 hadi miaka 19 wana uzito wa kupindukia huki Marekani ikiwa katika kiwango cha 21% cha watu wenye unene wa kupita kiasi.
Kwa upande mwingine tangu mwaka 200 pengo kati ya nchi maskini na tajiri kimepungua huku lakaini kiwango cha unene kikiendelea kupanda katika mataifa ya ukanda wa Pasific kutokana na kwamba vyakula vinavyoingia kutoka viwanda vya nje vinazidi kuchukua nafasi ya vyakula halisi vya ndani.
Kwa baadhi ya nchi wao ni kama matatizo haya mawili yanazidi kuwakabili ambapo mataifa yanahangaika kupata suluhu.
UNICEF imesema kwamba kwa baadhi ya sehemu hasa zile zenye changamoto za usalama mdogo na vita mashirika ya misaada yamekuwa yakitumia nafasi hii kusambaza vyakula vya viwandani bila kujua kuwa wanachangia kuendelea kuwepo kwa tatizo hilo la unene wa kupindukia.
UNICEF imezitaka serikali za mataifa kuchukua hatua za maksudi ikiwa ni pamoja na kuweka kanuni kali za kupunguza kiwango cha usambaji wa vyakula hivyo pamoja na ushuru kwa bidhaa zenye sukari nyingi na vyakula vingine visivyo na ubora.