1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN kupigia kura azimio la suluhisho la mataifa mawili

12 Septemba 2025

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa litapiga kura leo Ijumaa kuunga mkono azimio la New York kuamua iwapo litaunga mkono suluhisho la mataifa mawili kati ya Israel na Palestina bila kuwahusisha wanamgambo wa Hamas.

USA New York 2024 | Benjamin Netanjahu | Baraza kuu la Umoja wa Mataifa
UN kupigia kura azimio la suluhisho la mataifa mawili kati ya Israel na Paletina Picha: Charly Triballeau/AFP/Getty Images

Licha ya Israel kukosoa mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa miaka miwili kwa kile ilichosema ni kushindwa kwa Umoja huo kukosoa mashambulizi ya Oktoba 7 mwaka 2023 yaliyofanywa na Hamas nchini Israel, azimio hilo lililopendekezwa na Ufaransa na Saudi Arabia halina mjadala.

Azimio, linatoa wito wa hatua za pamoja kuchukuliwa kumaliza vita vya Gaza, kufikia suluhu ya kudumu ya mzozo wa Israel na Palestina kwa utekelezaji wa suluhu ya mataifa hayo mawili.

Rais wa Baraza hilo Annalena Baerbock amesema kanda ya mashariki ya kati haihitaji migogoro zaidi inachohitaji ni juhudi za kidiplomasia kuelekea amani.

"Kikao hiki cha 80 si kikao cha kawaida. Kuongezeka kwa vita ni jambo la kutia wasiwasi na natoa wito kwa pande zote kujizuwia. Kama inavyotakiwa na makubaliano yetu ya Umoja wa Mataifa, Uhuru na maeneo ya nchi wanachama ni lazima yaheshimiwe na yasikiukwe na nchi wanachama.Hatuhutaji vita zaidi Mashariki ya Kati, tunahitaji hatua za kidiplomasia zinazotuelekeza katika usitishwaji kamili wa vita, kuimarika kwa hali ya kibinaadamu kwa watu wa Gaza na kuachiwa kwa mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas"

Ujerumani imesema italiunga mkono azimio hilo japokuwa haiamini kama ni wakati sahihi wa kuitambua Palestina kama taifa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW