UN: kupigia kura rasimu ya kusitisha mapigano Gaza
12 Desemba 2023Hatua hii ikiwa ni miezi miwili tangu kuanza kwa mgogoro kati ya Israel na Hamas, baada ya Marekani kutumia kura yake ya turufu kuzuwia hatua hiyo kuchukuliwa, katika Baraza la Usalama la Umoja huo.
Hakuna nchi iliyo na nguvu ya kura hiyo ya turufu katika nchi 93 wanachama wa Baraza hilo ambalo linatarajiwa kuipigia kura rasimu inayooana na ile iliyopingwa na Marekani wiki iliyopita ndani ya Baraza la Usalama lililo na wanachama 15.
Soma pia:Israel inaweza kulitokomeza kabisa kundi la HamasI
Azimio za Baraza hilo hazina uzito wowote wa kisheria lakini zina nguvu za kisiasa na zinaashiria maoni ya dunia katika vita vinavyoendelea katika ukanda wa Gaza.
Wizara ya afya katika ukanda huo imesema hadi sasa wapalestina zaidi ya elfu 18,000 wameuwawa wakiwemo wanawake na watoto.