UN: Mamia ya watu huenda waliuawa El- Fasher
31 Oktoba 2025
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari hii leo mjini Geneva, msemaji wa Ofisi ya Haki ya Binadamu ya Umoja wa Mataifa amesema wanakadiria idadi ya vifo vya raia na wale waliotekwa wakati wa uvamizi huo wa RSF na njia za kutoka mjini huo huenda ikafikia mamia na kuelezea ushahidi wa mauaji makubwa ya kiholela.
Kuna ushahidi wa kubakwa kwa watu wasioungua wanawake 25
Magango amesema ofisi hiyo imepokea ushuhuda kutoka kwa wafanyakazi wa mashirika ya misaada kwamba watu wasiopungua wanawake 25 walibakwa na magenge wakati wapiganaji wa RSF walipoingia kwenye kambi za watu waliopoteza makazi yao karibu na chuo kimoja kikuu.
Pia amewaambia waandishi wa habari kwamba mashuhuda wamethibitisha kuwa wapiganaji wa RSF waliwachagua wanawake na wasichana na kuwabaka kwa makundi wakiwa wamewaelekezea bunduki, na kulazimisha takriban familia 100 zilizopoteza makazi kuondoka eneo .