1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Machafuko ya Sahel yataongeza wakimbizi zaidi Ulaya

16 Juni 2022

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi amesema machafuko katika eneo la Sahel yanaweza kuongeza idadi ya wakimbizi barani Ulaya.

Mali | G5 Sahel Militärallianz
Picha: Hans Lucas/IMAGO

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi amesema Ulaya inapaswa kuwa na wasiwasi zaidi kutokana na watu wengi kutoka eneo la kanda ya Sahel, wanaweza kutafuta kukimbilia upande wa kaskazini kujiepusha na machafuko, kadhia ya mabadiliko ya tabia nchi, ukame, mafuriko na tatizo la upatikanaji wa chakula lililosababishwa na vita vya Ukraine na Urusi.

Mkuu wa shirika UNHCR Filippo Grandi ametoa wito wa kufanyika juhudi zaidi za kustawisha amani ya ulimwengu katika kipindi hiki ambacho mizozo na vita kama vya Ukraine, Venezuela, Myanmar, Syria na kwingine duniani vikisababisha zaidi ya watu milioni 100 kuyakimbia makazi yao, iwe ndani ya taifa husika au hata nje ya mipaka ya taifa lao.

Idadi ya waliaochwa bila ya makazi inapindukia milioni 89 duniani.

Wakimbizi wa Burkina FasoPicha: imago images/Joerg Boethling

Katika ripoti yake ya mpya kwa mwaka 2021 ya Alhamis hii, UNHCR imebainisha zaidi ya watu milioni 89 wameachwa bila ya makazi kutokana na migogoro, mabadiliko ya tabia nchi,mapigano na ukiukwaji wa haki za binaadamu. Idadi inaonekana kuongezeka zaidi baada ya takribani watu milioni 12, kuikimbia Ukraine kufuatia uvamizi wa Urusi wa Februari 24.

Kwa mwaka huu pia ulimwengu unakabilina na shida ya chakula, Ukraine likiwa taifa muhimu kwa uzalishaji wa chakula barani Ulaya na vita vinavyoendelea sasa vinatatiza mauzo ya nafaka nje ya mipaka ya taifa hilo.

Hofu ya baa la njaa yaongezeka barani Afrika.

Umoja wa Afrika, ambao bara lake linategemea uagizaji wa ngano na vyakula vingine kutoka Ukraine, umeomba msaada wa kufanikishwa upatikanaji wa vyakula hivyo, ambavyo vimezuiwa katika eneo la nandari ya Ukraine  kutokana na jeshi la wanamaji la Urusi kuweka kizuizi katika eneo la Bahari ya Nyeusi.

Kwa zingatio la ripoti hii ya mwaka 2021, UNHCR inarekodi mwaka wa 15 kwa mfululizo wa ongezeko la kila mwaka la idadi ya watu wanaopoteza makazi yao ndani ya mataifa yao kupindukia zaidi ya milioni 53. Sababu ambazo zinatajwa kuwa ni kuongezeka kwa machafuko katika mataifa kama Myanmar, vita vya Ethiopia na hasa katika jimbo la Tigray, uasi wa makundi ya wenye itikadi kali, kwa zingatia la eneo la Sahel yakitajwa sana mataifa ya Burkina Faso na Mali.

Soma zaidi: UN: Zaidi ya wakimbizi 36,000 waingia Niger mwaka huu

Kamishna Grandi anasema kwa miaka kadhaa eneo la Sahel tayari limekuwa likikabliwa na ukame, njaa, shida ya elimu, tiba, uongozi duni na machafuko ya sasa yameongeza zaidi hali ngumu. Amesema kutoka na mazingira ya kijiografia ualaya lazia iwe na mashaka ya wimbi kubwa la watu kutoka katika eneo hilo. Na kisha akaongeza dunia lazima izingatie imekuwa ikikabliwa na tatizo lenye kusababisha ukimbizi kuliko hata vita vya Ukraine.

Chanzo: AP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW