1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

UN: Mapigano ya silaha nzito mjini El-Fasher nchini Sudan

12 Mei 2024

Mratibu wa masuala ya kiutu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Clementine Nkweta-Salami, ameelezea wasiwasi wake kuhusu ripoti kwamba silaha nzito zinatumika katika mapigano katika mji wa El-Fasher nchini Sudan

Soko la mifugo la El-Fasher lililoharibiwa kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali na kikosi cha RSF nchini Sudan
Soko la mifugo la El-Fasher lililoharibiwa na mashambulizi nchini SudanPicha: AFP

Katika taarifa, Nkweta-Salami amesema kuwa raia waliojeruhiwa wanakimbizwa hospitali huku wengine wakijaribu kukimbia mapigano katika eneo hilo la Darfur.

Mjumbe huyo amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa juu ya kuzuka kwa mapigano hayo huko El-Fashur licha ya wito wa mara kwa mara kwa wahusika katika mzozo huo kuacha kushambulia mji huo.

Maisha ya watu 800,000 yako hatarini El-Fasher

Nkweta-Salami alisisitiza kuwa ghasia hizo zinatishia maisha ya zaidi ya raia 800,000 wanaoishi mjini humo.

Mwezi Aprili, Marekani ilionya kuhusu hatari ya mashambulizi ya waasi wa kijeshi mjini humo, ambao ni kitovu cha misaada ya kibinadamu kinachoonekana kuwa kitovu cha mzozo mpya wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW