1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Mazungumzo ya bayoanuwai COP16 kuanza tena Februari

28 Novemba 2024

Mazungumzo magumu ya Umoja wa Mataifa ya kutafuta ufadhili wa kuzuia uharibifu wa mazingira yataanza tena mjini Roma mwezi Februari, baada ya mazungumzo ya mwezi Novemba nchini Colombia kumalizika bila makubaliano.

COP16 Cali
Mazungumzo hayo yatashughulikia masuala yaliyoachwa bila kutatuliwa kufuatia kusimamishwa kwa mkutano wa NovembaPicha: Camilo Rodriguez/REUTERS

Mkutano huo wa bayoanuwai utafanyika katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo - FAO kuanzia Februari 25 hadi 27 ili kushughulikia masuala "yaliyoachwa bila kutatuliwa kufuatia kusimamishwa kwa mkutano huo" mnamo Novemba 2.

Kongamano la ulinzi wa mazingira COP16 laanza Colombia

Washiriki 23,000 walimiminika mjini Cali nchini Colombia kwa mkutano mkubwa zaidi wa kilele kuhusu bayoanuwai uliolenga kulinda mazingiraasili dhidi ya ukataji miti, mabadiliko ya tabianchi na uchafuzi wa mazingira.

Mazungumzo yaliingia hadi usiku wa ziada lakini Colombia ambayo ndio ilishika uwenyekiti wa mkutano huo ikashindwa kupata idadi ya kutosha ya washiriki, baada ya wengi kuondoka mapema kurudi makwao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW