1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroEthiopia

UN: Mzozo wa Ethiopia wahofiwa kuenea nchi nzima

18 Septemba 2023

Ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu bado unafanywa nchini Ethiopia licha ya kuwepo makubaliano ya amani kaskazini mwa nchi hiyo.

Pande hasimu zilihusika na visa vya ukeukwaji wa haki za binadamu nchini Ethiopia
Pande hasimu zilihusika na visa vya ukeukwaji wa haki za binadamu nchini EthiopiaPicha: Minasse Wondimu Hailu/Anadolu Agency/picture alliance

Wataalamu wa masuala ya haki wa Umoja wa Mataifa wamesema hii leo kuwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu bado unafanywa nchini Ethiopia licha ya kuwepo makubaliano ya amani kaskazini mwa nchi hiyo.

Ukiukwaji mkubwa umeripotiwa kuongezeka maeneo ya Amhara na Oromia.

Mohamed Chande Othman, mkuu wa Tume hiyo ya wataalamu, amesema hali nchini Ethiopia ni mbaya mno na kumekuwa kukishuhudiwa vitendo vya ukatili, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu, na wameonya kuwa mzozo huo unaenea kote nchini Ethiopia na hivyo utulivu wa ukanda huo kuwa hatarini.

Novemba mwaka jana, makubaliano ya amani kati ya serikali ya shirikisho ya Ethiopia na waasi katika eneo la Tigray yalihitimisha mzozo wa kikatili uliodumu kwa miaka miwili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW