1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

UN: Nusu ya Wasudan wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula

28 Juni 2024

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa takriban watu milioni 26 nchini Sudan wanakabiliwa na viwango vya hatari vya uhaba wa chakula.

Sudan Agari | Wasudani wakisubiri msaada wa chakula.
Wasudan wakiwa katika msururu wa kupokea misaada ya kiutuPicha: Guy Peterson/AFP

Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNICEF, lile la chakula na kilimo FAO na la mpango wa chakula duniani WFP yamesema katika taarifa ya pamoja kuwa, nusu ya raia wa Sudan wanakabiliwa na changamoto ya kulisha familia zao.

Kwa mujibu wa ripoti iliyoandaliwa kwa kutumia kipimo cha kuboresha tathmini ya usalama wa upatikanaji wa chakula na mchakato wa kupitisha maamuzi, IPC, kuna hatari kubwa ya maeneo 14 nchini humo kukumbwa na baa la njaa iwapo vita kati ya jeshi na kundi la wanamgambo la RSF vitaaendelea.

Soma pia:Wataalamu wa UN watuhumu pande zinazopigana Sudan kutumia njaa kama silaha

IPC imeorodhesha maeneo ya mji mkuu Khartoum, Darfur, Kordofan na jimbo la El Gezira kama maeneo ambayo yanakabiliwa na changamoto ya uhakika wa kupata chakula.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW