1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Pengo laongezeka kati ya mataifa tajiri na maskini

11 Aprili 2026

UN imesema pengo kati ya mataifa tajiri na maskini linaongezeka huku hatua zilizokubaliwa na nchi nyingi mwaka jana, ikiwa ni pamoja na kurekebisha taasisi kuu za kifedha duniani, zikisalia kuwa ahadi tu.

Mahojiano na DW |Kristalina Georgieva
Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Kristalina GeorgievaPicha: DW

Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Kristalina Georgieva, amesema ripoti hiyo ilikuwa imetayarishwa kuboresha ukuaji wa kimataifa, lakini vita vya Iran vimevuruga mtazamo wa uchumi wa dunia.

Kwa upande wake, naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kiuchumi na kijamii Li Junhua, amesema mivutano ya kijiografia na kisiasa inazidisha changamoto katika nchi zinazoendelea kuvutia ufadhili.

Ameongeza kuwa huu ni wakati wa hatari sana kwa ushirikiano wa kimataifa, kwasababu masuala hayo ya kijiografia na kisiasa yanazidi kuchagiza mahusiano ya kiuchumi na sera za kifedha.

Ripoti hiyo imeashiria kuwa kuongezeka kwa vikwazo vya kibiashara pia kunachangia pengo hilo linaloongezeka.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW