1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

UN: RSF wamesababisha vifo vya zaidi ya watu 1000 Sudan

19 Desemba 2025

Wanamgambo wa kikosi cha RSF ambao wamekuwa vitani na jeshi la serikali kwa muda wa miaka miwili na nusu, walisababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000 wakati wa mashambulizi ya siku tatu waliyoyafanya mwezi Aprili.

Sudan | El-Fasher 2025 | RSF | Darfur
Kikosi cha wapiganaji wa RSF katika mji wa El-FasherPicha: Rapid Support Forces/AFP

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa jana.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu OHCHR imeeleza katika ripoti yake kwamba "ilirekodi mauaji ya raia 1,013 wakati wa mashambulizi ya RSF kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Zamzam kati ya Aprili 11 na 13."

Ripoti hiyo imeongeza kuwa zaidi ya wakimbizi 400,000 waliokuweko kwenye kambi hiyo walilazimika kukimbia wakati wa mashambulizi hayo ya siku tatu.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF yamesababisha takriban watu milioni 12 kuyahama makaazi yao nchini Sudan huku maelfu ya wengine wakikabiliwa na kitisho cha njaa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW