1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Sudan inakabiliwa na ghasia na uhaba wa misaada

16 Mei 2024

Wakaazi wa Sudan inayokumbwa na mzozo wamenaswa katika ghasia za kikatili na wanazidi kuwa katika hatari ya kukabiliwa na njaa kutokana na msimu wa mvua pamoja na vitendo vya kuzuiwa kwa misaada.

Darfur Sudan
Mkimbizi wa DarfurPicha: Unamid Handout/Albert Gonzalez F/picture alliance

Wakaazi wa Sudan inayokumbwa na mzozo wamenaswa katika ghasia za kikatili na wanazidi kuwa katika hatari ya kukabiliwa na njaa kutokana na msimu wa mvua pamoja na vitendo vya kuzuiwa kwa misaada.

Hayo yameelezwa na mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Clémentine Nkweta-Salami ambaye ameonya pia kwamba hali huko Sudan inaweza kuwa mbaya zaidi kwa kuwa nchi hiyo iko katika hatari ya kukabiliwa na njaa pamoja na magonjwa.

Makumi ya maelfu ya watu wamekufa na mamilioni ya wengine wameyakimbia makazi yao tangu vita hivyo vilipozuka Aprili mwaka jana kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha RSF. Umoja wa Mataifa umeonyesha wasiwasi unaoongezeka katika siku za hivi karibuni kutokana na ripoti za mapigano makali katika maeneo yenye wakazi wengi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW