JamiiLebanon
UN: Watu milioni 4 Lebanon wanahitaji msaada wa kibinadamu
6 Oktoba 2023Matangazo
Imran Riza amesema nusu ya watu hao hawatopata misaada kutokana na ukosefu wa ufadhili.
Tangu 2019, Lebanon imekuwa ikikabiliwa na mfululizo wa majanga. Wanasiasa wa nchi hiyo ambao wanalaumiwa kwa miongo kadhaa ya ufisadi na usimamizi mbovu wa mali ya umma, wamekuwa wakipinga mageuzi ya kiuchumi na kifedha yaliyoombwa na jumuiya ya kimataifa.
Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu amebainisha kuwa Lebanon imekuwa bila rais kwa karibu mwaka mmoja na taasisi zake nyingi hazifanyi kazi. Watu wanaohitaji msaada ni raia wa Lebanon, wahamiaji pamoja na wakimbizi kutoka Syria na Palestina.