1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Takriban watu milioni 4 wapoteza makao eneo la Sahel

11 Oktoba 2025

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, takriban watu milioni wamepoteza makazi yao katika eneo la Sahel, barani Afrika na umetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuhakikisha misaada inapatikana kwa haraka.

Burkina Faso UNHCR- Abdouraouf Gnon-Konde
Mkurugenzi wa UNHCR kanda ya Afrika Magharibi na Kati, Abdouraouf Gnon-KondePicha: Richard Tiéné/DW

Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi katika kanda ya Afrika Magharibi na Kati Abdouraouf Gnon-Konde, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi kwamba waliopoteza makaazi yao wanatokea  Burkina Faso, Mali, Niger na nchi jirani ya hizo, na idadi yao inakaribia theluthi mbili zaidi, ikilinganishwa na idadi ya miaka mitano iliyopita.

Gnon-Konde amesema hali hii inaashiria ukosefu wa usalama, upatikanaji mdogo wa huduma na njia za kukidhi maisha, pamoja na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW