JangaAfrika
UN: Tahadhari ya mapema ingelipunguza madhara Libya
14 Septemba 2023Matangazo
Mkuu wa Shirika la masuala ya hali ya hewa la Umoja huo, WMO petteri Taalas amewaambia waandishi wa habari mjini geneva kwamba, kama mifumo hiyo ingekuwa inafanya kazi sawasawa, wangeweza kuwahamisha wakazi na kuepusha vifo na majeruhi kama inavyoshuhudiwa sasa.
Taalas amesema kama kungekuwa na mifumo ya hali ya hewa inayofanya kazi kama kawaida, wangekuwa wametoa tahadhari na mamlaka za dharurazingeweza kuwahamisha wakazi.
Soma pia:Juhudi za kuisaidia Libya zashika kasi
Saalas ametoa matamshi hayo baada ya upande wa Mashariki wa Libya kukumbwa na mafuriko ya kiwango cha Tsunami mwishoni mwa wiki iliyopita na kuua karibu watu 4,000, huku maelfu wakiwa hawajulikani walipo.