1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Ulimwengu upo katika wakati hatari zaidi katika historia

Sylvia Mwehozi
18 Oktoba 2024

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ameonya kwamba ulimwengu upo katika wakati hatari zaidi katika historia huku hali ya kutozingatia na kutoheshimu sheria za kimataifa ikifikia kiwango cha juu.

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk
Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk Picha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/picture alliance

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ameonya kwamba ulimwengu upo katika wakati hatari zaidi katika historia huku hali ya kutozingatia na kutoheshimu sheria za kimataifa ikifikia kiwango cha juu.

Soma: Baraza la Haki la UN lataka Israel kuwajibishwa kwa uhalifu wa kivita huko Gaza

Türk ameeleza kwamba migogoro inazidi kuenea huku sheria na haki za binadamu zikizidi kukanyagwa. Mkuu huyo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amezikosoa vikali mamlaka za Israeli kwa kuruhusu Wapalestina huko Gaza kufikia viwango vya janga la njaa lakini pia ametaja ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Ukraine, Sudan, Haiti na Myanmar.

Turk alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha ripoti yake katika kamati inayohusika na haki za binadamu ya Baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW