1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Urusi inafanya uhalifu dhidi ya binadamu Ukraine

1 Novemba 2024

Hatua ya Urusi kuwatesa raia wa Ukraine na wafungwa wa kivita ni uhalifu dhidi ya binadamu. Haya ni kwa mujibu wa wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

Jela katika eneo la Kherson, Ukraine
Jela katika eneo la Kherson, UkrainePicha: Igor Burdyga/DW

Erik Mose ambaye ni mwenyekiti wa tume huru inayochunguza ukiukaji wa haki za binadamu nchini Ukraine amewaambia waandishi wa habari kuwa jopo lake limepata kuwa wanawake kwa wanaume katika mikoa yote ya Ukraine iliyo chini ya udhibiti wa Urusi, wamekuwa wakiteswa.

Mpango wa Umoja wa Mataifa Urusi haukutoa tamko lolote kuhusiana na ripoti ya tume hiyo ya watalaam wa Umoja wa Mataifa.

Uchunguzi Ukraine na ndani ya Urusi

Mose amesema kwamba Ukraine pamoja na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC wanafanya uchunguzi kuhusiana na uwezekano wa kufanyika kwa matukio ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu nchini humo na huenda kama tume wakaitishwa ushahidi.

Mose amesema makamishena wake wamechunguza ripoti kutoka jela 41 tofauti katika maeneo tisa yaliyokaliwa na Urusi nchini Ukraine na maeneo 8 nchini Urusi.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Kimataifa kuhusu haki nchini Ukraine, Erik MosePicha: Igor Burdyga/DW

Amesema kwamba tume hiyo imebaini kuwa mateso ambayo hufanywa katika jela za Urusi yanafanywa pia katika jela zilizoko katika maeneo waliyoyakalia nchini Ukraine.

Mose ameongeza kuwa wamepata ushahidi wa ziada wa udhalilishaji wa kingono kutumika mara kwa mara kama njia ya mateso.

Athari za kisaokolojia miongoni mwa wafungwa

Kamishena wa tume hiyo Vrinda Gover amesema wafungwa walibakwa, wakalazimishwa kuketi uchi kwa muda mrefu na kukaguliwa na kufanyiwa mambo mengine mengi zaidi.

Mojawapo ya kituo cha wafungwa KhersonPicha: Igor Burdyga/DW

Gover amesema wahanga wengi wameripoti kudhalilishwa kingono na kwamba wameathirika kisaikolojia kutokana na mateso hayo.

Kamishena mwengine Pablo de Greiff amewaambia waandishi wa habari kuwa kwa sasa wana ushahidi wa itifaki ya Urusi iliyohusika na uratibu na kuwezesha mateso katika jela na vituo vya kuwazuia wafungwa.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi