1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

UN: Urusi inatumia mateso ya kikatili nchini Ukraine

25 Septemba 2023

Tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Ukraine imesema Urusi imekuwa ikitumia mifumo ya mateso ya kikatili.

Chumba cha chini cha ardhini katika kiutuo cha polisi eneo la Balakliia, Kharkiv nchini Ukraine kilichokombolewa na Ukraine kutoka kwa vikosi vya Urusi. Inadaiwa kuwa chumba hicho kilikuwa kikitumiwa na wanajeshi wa Urusdi kuwatesa Waukraine.
Chumba cha chini cha ardhini katika kiutuo cha polisi eneo la Balakliia, Kharkiv nchini Ukraine kilichokombolewa na Ukraine kutoka kwa vikosi vya Urusi. Inadaiwa kuwa chumba hicho kilikuwa kikitumiwa na wanajeshi wa Urusdi kuwatesa Waukraine.Picha: Kyodo/picture alliance

Kulingana na Umoja wa Mataif, mifumo hiyo ni pamoja na kuwatesa wahanga hadi kifo. Mwenyekiti wa Tume hiyo Erik Møse ameliambia hii leo Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi.

Tume hiyo ilitembelea sehemu kadhaa za Ukraine zilizokuwa zikishikiliwa na vikosi vya Urusi hususan mikoa ya Kherson na Zaporizhzhia.

Na iligundua kuwa mateso hayo yalifanywa hasa katika magereza yaliyo chini ya udhibiti wa mamlaka ya Urusi na kwamba yanaweza kuchukuliwa kama uhalifu dhidi ya binaadamu.

Urusi ilipewa fursa ya kujibu madai hayo lakini haikuwa na mwakilishi katika kikao hicho. Moscow imekuwa ikikanusha mara kadhaa kufanya ukatili au kuwalenga raia katika vita vyake nchini Ukraine.

Makombora ya Urusi yamjeruhi mtu mmoja katika bandari ya Odessa nchini Ukraine

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW