1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Vifo viliongezeka kwa asilimia 72 mwaka 2023

18 Juni 2024

Mizozo ya kivita ilichangia ongezeko la vifo vya raia kwa asilimia 72 mwaka 2023.

Volker Turk, mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa
Volker Turk, mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa MataifaPicha: Pierre Albouy/KEYSTONE/picture alliance

Mkuu wa Shirika la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema vifo vya raia vilivyosababishwa na mizozo ya kivita viliongezeka kwa asilimia 72 mwaka uliopita na kuonya juu ya uwiano wa wanawake na watoto wanaouawa.

Amesema hayo kwenye ufunguzi wa kikao cha Baraza la Haki za Binaadamu la umoja huo na kuongeza kuwa takwimu zilizokusanywa na ofisi yake mwaka 2023 zilionyesha uwiano wa vifo vya akina mama uliongezeka mara mbili na vya watoto viliongezeka mara tatu.

Turk aidha amesema misaada ya kibinaadamu ilipungua kwa dola bilioni 40.8 kote ulimwenguni na ni asilimia 16.1 tu ndio iliyotolewa.

Amesema huo ulikuwa ni upungufu mkubwa zaidi wa mwaka kwa mwaka, tangu mwaka 2009.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW