1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMyanmar

UN wachunguza kupotea kwa makaazi ya maelfu ya watu Myanmar

23 Mei 2024

Wachunguzi wa uhalifu wa kivita wa Umoja wa Mataifa wamesema leo kuwa wanafuatilia mapigano yanayozidi kuongezeka katika Jimbo la Rakhine nchini Myanmar linalokumbwa na migogoro.

Wanajeshi wa Thailand wakishika doria karibu na kituo cha ukaguzi cha mpaka wa Tak
Wanajeshi wa Thailand wakishika doria karibu na kituo cha ukaguzi cha mpaka wa TakPicha: AFP

Wachunguzi wa uhalifu wa kivita wa Umoja wa Mataifa wamesema leo kuwa wanafuatilia mapigano yanayozidi kuongezeka katika Jimbo la Rakhine nchini Myanmar linalokumbwa na migogoro na pia kuchunguza ripoti kwamba maelfu ya watu kutoka jamii ya walio wachache wanaoteswa wamekimbia makazi yao.

Katika taarifa, Mfumo Huru wa Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kwa Myanmar (IIMM) umesema unafuatilia kwa karibu matukio yanayojitokeza katika eneo la Rakhine na kufanyia tathmini kama uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita umetekelezwa.

Soma pia: Mapigano yazuka kwenye mpaka wa Myanmar na Thailand

Katika taarifa, IIMM, imesema inachunguza ripoti nyingi za mapigano makali kati ya jeshi la Myanmar na Jeshi la Arakan, pamoja na kuongezeka kwa ghasia na uharibifu wa mali katika mji wa Buthidaung.

IIMM imesema kuwa vurugu zimeripotiwa kusababisha kupoteza makazi kwa maelfu ya raia wa jamii ya Rohingya na pia zimeathiri jamii za Rakhine na Kihindi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW