1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Wafanyakazi 35 wa mashirika ya misaada wauawa Nigeria

19 Agosti 2022

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuwepo usalama wa wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada kwenye eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria

Nigeria | Wasserknappheit in Maiduguri
Picha: Gilbertson/ZUMAPRESS/picture alliance

Kulingana na Umoja wa Mataifa, wapiganaji wa jihadi wamesababisha vifo vya wafanyakazi 35 wa mashirika ya kutoa misaada eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa, tangu mwaka 2016, wafanyakazi 22 wameuawa na wengine 28 wametekwa nyara.

Takribani watu 40,000 wamekufa katika eneo hilo na kiasi ya milioni mbili wamelazimika kuyakimbia makaazi yao tangu mwaka 2009, wakati kundi la Boko Haram lilipoanzisha mashambulizi.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu misaada ya kiutu, OCHA, limesema kulingana na msingi wa takwimu za usalama wa wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada, tangu mwaka 2016, wafanyakazi 35 wameuawa katika eneo hilo.

Matthias Schmale, mratibu wa OCHA nchini Nigeria, amewapongeza wafanyakazi hao kwa kuokoa maisha ya mamilioni ya watu kwenye eneo hilo lisilo na utulivu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW