1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Wafanyakazi 40 wa misaada wameuawa Myanmar tangu 2021

6 Julai 2023

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema wafanyakazi wa misaada wapatao 40 wameuawa nchini Myanmar tangu jeshi lilipoiondoa serikali ya kidemokrasia ya Aung San Suu Kyi mwaka 2021.

Myanmar | Militär
Picha: AFP/Getty Images

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema wafanyakazi wa misaada wapatao 40 wameuawa nchini Myanmar tangu yalipofanyika mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani kiongozi aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia Aung San Suu Kyi mwaka 2021.

Katika ripoti yake kwa Baraza la Haki za Kibinadamu, Turk amelaani mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya wafanyakazi wa misaada, ambao wanashirikiana na mashirika ya ndani, huku kukiwa na mapigano kati ya jeshi lililounga mkono mapinduzi na wapinzani wake. Wanajeshi wanatuhumiwa kuwaua raia na kuharibu miundombinu muhimu.

Turk ameongeza kuwa vitendo hivyo ni sehemu ya harakati za makusudi zinazolenga kuzuia misaada na kukandamiza haki za msingi na kuminya uhuru wa idadi kubwa ya watu wa Myanmar ambapo Umoja huo umeonya kuwa matendo hayo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW