1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Wanamgambo wa RSF walifanya mauaji ya kimbari el-Fasher

20 Februari 2026

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wanasema kampeni ya uharibifu iliyofanywa na wanamgambo wa RSF mnamo Oktoba dhidi ya jamii zisizo za Kiarabu ndani na karibu na mji mmoja huko Darfur, inaonesha ishara za "mauaji ya kimbari."

Mpango maalum wa kutafuta ukweli wa Umoja wa Mataifa umesema kuwa wanamgambo wa RSF ambao wanapambana na jeshi la Sudan, walifanya mauaji ya halaiki na ukatili mwengine katika mji wa el-Fasher baada ya uvamizi wa miezi 18.

Umoja wa Mataifa unasema ni wakati huo ndipowanamgambo hao walipoweka mipango ya kuziangamiza jamii zisizo za Kiarabu, hasa makabila ya Zaghawa na Fur.

Maafisa hao wa Umoja wa Mataifa wanasema maelfuya raia waliuwawa baada ya RSF kuuteka mji wa el-Fasher.

Ni asilimia 40 tu ya raia wa mji huo waliofanikiwa kukimbia wakiwa hai, ambapo maelfu miongoni mwao waliuwawa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW