1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

UN: Washirika wanaopeana silaha Sudan walaumiwa

13 Novemba 2024

Mkuu wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarlo, amewalaumu washirika wanaoviunga mkono vikosi vya kijeshi vinavyopigana nchini Sudan kwa kuvipa silaha.

Mkuu wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarlo
Mkuu wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarloPicha: Eskinder Debebe/Xinhua News Agency/picture alliance

DiCarlo aliliambia Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa kwamba mapigano hayo yanatakiwa yasimamishwe mara moja.

Amesema vikosi hivyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 24,000 na pia vimesasbabisha mzozo mbaya zaidi duniani wa watu kulazimika kuyahama makazi yao kwa ajili ya kukimbia vita amesisitiza kwamba matukio hayo hayakubaliki na yanakiuka sheria.

 Mkuu wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarlo ametoa wito wa kuzilazimisha pande zinazopigana nchini Sudan zikubali kufanya mazungumzo.

Hivi majuzi Umoja wa Mataifa ulitahadharisha kuwa nchi hiyo iko ukingoni kutmbukia kwenye baa la njaa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW