1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Watu 87 walizikwa katika kaburi la pamoja Darfur

Hawa Bihoga
13 Julai 2023

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema takriban watu 87 wakiwemo wa kabila la Masalit, walizikwa katika kaburi la pamoja huko Darfur Magharibi mwa Sudan, Kikosi cha Msaada wa dharura RSF kikishutumiwa.

Schweiz, Genf: Volker Türk, UN-Hochkommissar für Menschenrechte
Picha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/dpa/picture alliance

Taarifa ya Umoja wa Mataifa inaonesha kwamba watu katika eneo hilo walilazimika kutupa hovyo miili ya watu, ikiwa ni pamoja na ya wanawake na watoto katika maeneo ya wazi karibu na mji wa magharibi wa El-Geneina kati ya Juni 20 na 21.

Baadhi ya watu walikufa kutokana na majeraha ambayo hayajatibiwa, wakati wa wimbi la ghasia za RSF na wanamgambo washirika baada ya kuuawa kwa gavana wa eneo hilo.

Kamishna wa Haki za Kibinadamu Volker Turk, katika taarifa hiyo amelaani vikali mauaji ya raia na watu binafsi na kushangazwa na hali ya miili hiyo, familia na jamii kwa ujumla namna ambavyo imetendewa ukatili bila huruma na bila kuheshimu utu na kutoa wito wa kufanyika haraka kwa uchunguzi wa kina, dhidi ya dhuluma hizi.

Soma pia:HRW yasema mauaji ya kutisha yanatokea Darfur

Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja ni sehemu gani ya waliofariki walikuwa Masalit.

Huku umwagaji damu unaochochewa na ukabila ukiongezeka katika wiki za hivi karibuni sambamba na vita kati ya makundi hasimu ya kijeshi ambayo yalizuka mwezi Aprili.

 Msemaji wa RSF hakupatikana kwa haraka kuweza kuzungumzia shutuma hizo.

Msemaji wa jeshi Brigedia Jenerali Nabil Abdullah amesema tukio hilo "linaongeza viwango vya uhalifu wa kivitana aina hiyo ya uhalifu unapaswa kuchukuliwa hatua kali za uwajibikaji.

Hali ya kiutu katika eneo hilo bado changamto

Darfur ilikuwa eneo la vita vya mauaji ya halaiki mwanzoni mwa miaka ya 2000, wakati makundi ya kikabila ya uwasi, wakiishutumu serikali inayoongozwa na Waarabu huko Khartoum.

Umoja wa Mataifa hapo jana Jumatano ulisema karibu miezi mitatu ya vita nchini Sudan imeathiri zaidi ya watu milioni tatu, na kutoa wito kwapande zinazozozana kukabiliana na "uwajibikaji".

Mzozo wa wakimbizi wa Sudan

02:20

This browser does not support the video element.

Takwimu za shirkia la Uhamaji la Umoja huo IOM zilionyesha kuwa zaidi ya watu milioni 2.4 sasa wamekimbia makazi yao ndani ya Sudan, wakati karibu 724,000 wametoroka kuvuka mipaka ya nchi hiyo, katika mkondo unaoendelea kuongezeka.

"Watu 930 wanaishi hapa, familia 136, pamoja na watoto 420, na pia kuna wanawake wajawazito 23 hadi 24, 6 kati yao tayari wamejifungua."

Alisema Mohamed Khaled kutoka shirika la msaada Sudan amesema katika eneo hilo ambalo kabla vita ilikuwa ni chuo msaada wa kimataifa ni haba.

"Kwa kuongezea kuna karibu wagonjwa wa magonjwa sugu takriban 150 ikiwemo shinikizo la damu na kisukari, na tuna watoto wachanga 20."

Katika kuikabili hali ya kutuliza vita hivyo Misri chini ya rais Abdel Fattah el-Sissinayo imejitosa katika kutafuta njia za kumaliza vita hivyo, ambapo leo imekuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani ya viongozi wa juu wa mataifa 6 ya Afrika ikiwemo Ethiopia, Sudan Kusini, Chad, Eritrea, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Libya.

Soma pia:Sudan yakataa kushiriki mkutano wa IGAD na Kenya

Baadhi ya mataifa ya Magharibi ikiwemo Uingereza tayari yamekwisha chukua hatua ikiwemo kutangaza vikwazo kwa wafanyabiashara ambao wanachochea mzozo huo na baadhi ya watu katika pande zote mbili za mzozo.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW