1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Watu Bilioni 1 hatarini kuambukizwa Kipindupindu

19 Mei 2023

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa watu bilioni moja katika mataifa 43 duniani wapo katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu.

Msumbuji l Mji Mkuu, Maputo ulipokumbwa na Kipindupindu Machi mwaka 2023
Mazingira yaliyo na uchafu ni chanzo kikubwa cha mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu Picha: Romeu Silva/DW

Shirika hilo limesema licha ya kwamba mripuko wa ugonjwa huo unaweza kuzuiwa, ufadhili unakosekana.

Umoja huo umesema unahitaji dola milioni 640 kupambana na ugonjwa huo, lakini umesema muda zaidi unaochukuliwa kuudhibiti kunaifanya hali kuwa ngumu zaidi.

Henry Gray, meneja wa Shirika la Afya Duniani, katika kitengo cha kushughulikia ugonjwa huo, amesema hadi sasa nchi 24 zimeripoti mripuko wa kipindipindu ikilinganishwa na mataifa 15 yaliyoripoti hilo mwezi Machi mwaka jana.

Gray amesema hatari ya mripuko huo inasababishwa na ongezeko la umasikini, migogoro, mabadiliko ya tabia nchi pamoja na watu kukosa makaazi yao kufuatia sababu hizo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW