1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Watu bilioni 1.1 wakabiliwa na umaskini

17 Oktoba 2024

Zaidi ya watu bilioni moja duniani wanaishi katika umaskini mkubwa.

Baba na mwanaye wakila chakula katika kitongoji chao kule Colombo, Sri Lanka
Baba na mwanaye wakila chakula katika kitongoji chao kule Colombo, Sri LankaPicha: Eranga Jayawardena/AP/picture alliance

Haya ni kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP iliyotolewa Alhamisi. Ripoti hiyo inasema watoto ni zaidi ya nusu ya wanaoathirika na hali hiyo.

Ripoti hiyo inaonesha kwamba viwango vya umaskini viko juu kwa mara tatu zaidi katika nchi zinazokabiliwa na vita, kwani mwaka 2023 ndio mwaka ulioshuhudia machafuko mengi zaidi kote duniani tangu Vita vya Pili vya Dunia.

India ndiyo nchi iliyo na idadi kubwa ya watu maskini kupindukia ambapo watu milioni 234 kati ya idadi jumla ya watu bilioni 1.4 nchini humo wanaishi katika hali hiyo.

Inafuatiwa na Pakistan, Ethiopia, Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Nchi hizo tano kwa pamoja zina karibu nusu ya hao watu bilioni 1.1 maskini duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW