1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

UN: Watu milioni 8 wamekimbia Ukraine tangu uvamizi wa Urusi

7 Februari 2023

Mratibu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na misaada ya dharura, Martin Griffiths amesema watu wapatao milioni 8 wamekimbia kutoka nchini Ukraine tangu Urusi iliopivamia Ukraine mwaka mmoja uliopita.

UN-Nothilfekoordinator Griffiths
Picha: Martial Trezzini/KEYSTONE/dpa/picture alliance

Griffiths amesema watu wengine milioni 5.3 wamegeuka kuwa wakimbizi wa ndani. Mkuu huyo wa uratibu wa masuala ya kiutu wa Umoja wa Mataifa ameliambia Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba watu takriban milioni17.6 sawa na asilimia 40 ya wakaazi Ukraine wanahitaji msaada ambapo takriban dola bilioni 3.9 zinahitajika.

Kulingana na Umoja wa Mataifa takriban watu 7,000 wameuawa tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mwaka uliopita.Vita vya Urusi nchini humo vimesababisha idadi kubwa kabisa ya wakimbizi ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu kumalizika vita vikuu vya pili.