1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUturuki

UN yachangisha robo ya fedha za msaada kwa Uturuki

31 Machi 2023

Umoja wa Mataifa umesema leo kwamba umechangisha robo ya fedha unazohitaji kwa ajili ya shughuli za kiutu nchini Uturuki baada ya tetemeko la ardhi lililowauwa zaidi ya watu 55,000

Erdbeben in der Türkei - Kahramanmaras
Picha: Abed Alrahman Alkahlout/ZUMA/IMAGO

Kulingana na msemaji wa shirika la misaada ya kiutu la Umoja wa Mataifa, Jens Laerke aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, kufikia sasa wafadhili wamechangisha dola milioni 268 kati ya dola bilioni moja zinazotakiwa.

Marekani, Kuwait, Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa, CERF na Saudi Arabia kwa sasa ndio waliochangisha kiasi kikubwa cha fedha kufikia sasa.

Laerke anasema Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya misaada wamefanikiwa kuwasaidia zaidi ya watu mioni 4.1.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW