1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yahimiza hatua za kupambana na chuki za kidini

12 Julai 2023

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio linaloyahimiza mataifa duniani kuchukua hatua za kupambana na chuki za kidini zinazochochea ubaguzi

Pakistan: Anti-Sweden demonstration in Islamabad
Picha: Raja Imran/Pacific Press/picture alliance

Pendekezo la azimio hilo liliwasilishwa na Pakistan baada ya kisa cha kuchomwa hadharani kwa kitabu kitakatifu kwa Waislamu cha Qur'an kilichotokea hivi karibuni nchini Sweden na kuzusha hasira miongoni mwa waumini wa dini hiyo duniani.

Soma pia: Iran yasitisha kumpeleka balozi wake nchini Sweden kupinga kitendo cha kuchomwa kwa Quran

Kwenye kikao cha baraza hilo kinachoendelea mjini Geneva, mataifa 28 yamepiga kura za ndiyo kuidhinisha azimio hilo huku nchi 12 zikilipinga na nyingine 7 zikijizuia kupiga kura.

Chini ya azimio hilo, mataifa ulimwenguni yanatolewa mwito wa kuzipitia upya sheria na kuziba mianya inayoweka vizingiti vya kushughulikiwa kwa matendo yanayochochea chuki za kidini.

Hata hivyo, azimio hilo linapingwa vikali na mataifa mengi ya Magharibi yakiongozwa na Marekani yanayosema linatishia uhuru wa watu kujieleza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW