UN yahofia mzozo wa chakula Sahel
11 Januari 2023Watu wengine milioni tano zaidi wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa usalama wa upatikanaji wa chakula, huku Burkina Faso, Niger na Nigeria zikiwa miongoni mwa nchi zilizoathiriwa sana.
Ripoti ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa kwa baraza la usalama la umoja huo jana Jumanne inasema miongoni mwa mambo yanayosababisha mzozo huo ni uhaba wa ngano na mbolea uliotokana na vita vya Ukraine, kukosekana usalama katika ukanda wa Sahel, hasa nchini Burkina Faso na Mali, na ongezeko la athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Ripoti hiyo pia imesema hali ya kibinadamu, hususan katikati mwa Sahel, bado ni mbaya na inazidishwa makali na kupanda kwa bei za chakula na nishati, pamoja na majanga yanayohusiana na hali ya hewa, yaliyosababishwa na mvua kubwa, mafuriko na uchafuzi wa maji.