1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

UN yaitaka Uingereza kufirikia upya sheria yake ya uhamiaji

Sylvia Mwehozi
23 Aprili 2024

Wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayoshugulikia wakimbizi na haki za binadamu wameitolea mwito Uingereza wa kutafakari upya juu ya sheria yake ya kuwapeleka waomba hiafdhi nchini Rwanda.

Volker Türk, Mkuu wa Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa
Volker Türk, Mkuu wa Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa MataifaPicha: KHALED DESOUKI/AFP

Mkuu wa shirika la Wakimbizi la UNHCR Fillipo Grandi na Kamishina Mkuu wa haki za binadamu Volker Turk, wamesema kuwa muswada wa sheria hiyo uliopitishwa jana usiku, kwa kiasi kikubwa unazuia uwezekano wowote wa kukataa kupelekwa wakimbizi Rwanda hata kama wahamiaji hao watakabiliwa na hatari wakati wa mchakato huo.

Aidha, pia wameeleza kuwa hali za watu huenda zisitiliwe maanani kabla ya kupelekwa Rwanda, kinyume na sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW