UN yakaribisha hatua ya kusitisha mapigano kwa muda Gaza
16 Juni 2024Umoja huo lakini kupitia msemaji wa shirika lake la kuratibu misaada ya dharura OCHA Jens Laerke limetoa wito wa hatua zaidi kuchukuliwa kutozuwia misaada zaidi kuingizwa katika maeneo yaliyo na uhitaji mkubwa wa msaada huo wa kibinaadamu.
Israel kusitisha mapigano kwa muda kila siku Gaza
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na makundi ya misaada ya kiutu yamekuwa yakitahadharisha kuhusu ukosefu wa chakula na mahitaji mengine muhimu katika Ukanda wa Gaza yaliyosababishwa na kuzuwiwa kwa misaada hiyo na kufungwa kwa njia ya kupitishia misaada hiyo ya Rafah inayopakana na Misri tangu Israel walipodhibiti eneo hilo mwanzoni mwa mwezi Mei.
Jeshi la Israel lilitangaza kusitisha mapigano hayo kila siku katika eneo hilo la Kusini mwa Rafah kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa moja jioni. Hatua hiyo itafanyika kila siku hadi taarifa nyengine itakapotolewa.