1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

UN yakutana kujadili azimio la Kyiv na washirika wake

Hawa Bihoga
22 Februari 2023

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa linakutana siku mbili kabla ya kumbukumbu ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, huku Kyiv na washirika wake wakitaraji uungwaji mkono kwa azimio linalotaka "haki na amani ya kudumu".

USA UN-Sicherheitsrat
Picha: Loey Felipe/UN Photo/Xinhua/IMAGO

Rasimu ya azimio la Kyiv na washirika wake lililofadhiliwa na baadhi ya nchi 60, inatarajiwa kupigiwa kura baada ya kufungwa kwa mjadala ambao utazamiwa kumalizika hapo kesho Alkhamisi.

Nakala ya rasimu inasisitiza haja ya kufikiwaharaka iwezekanavyo haki na amani ya kudumu nchini Ukraine, kulingana na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Kama maazimio ya awali, inathibitisha tena "ahadi ya Umoja wa Mataifa kwa uhuru, umoja na kuheshimu mipaka ya  Ukraine" na kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa uhasama.

Soma pia:Mkutano wa Munich wamalizika kwa miito ya kuisaidia Ukraine

Rasimu hiyo ambayo tofauti na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hayaundi makubaliano ya sheria katika pande zinazohasimiana, yanayoitaka Urusi kuondoa mara moja, kikamilifu na bila masharti vikosi vyake nchini Ukraine.

Kyiv inatarajia kupata uungwaji mkono wa mataifa mengi kama ilivyokuwa mwezi Oktoba, wakati nchi 143 zilipopigia kura azimio la kulaani Urusi kunyakuwa maeneo kadhaa ya Ukraine.

Zelenskyy:Urusi imeendeleza mashambulizi makali

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema vikosi vya Urusi vimeendeleza mashambulizi katika baadhi ya maeneo ikiwemo mkoa wa Kherson na kuuwa watu kadhaa huku wengine wakijeruhiwa.

Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Ukrainian Presidential Press Office/AP/dpa

Amesema taarifa zinatotoka katika maeneo ya Donetsk na Luhansk, zinaleta hisia za tofauti, lakini vikosi vyake vinaendelea na mapambano katika uwanja wa vita.

"Tunafanya kila kitu kuzuia mashambulio ya adui huko ambayo ni makali na ya mara kwa mara." Alisema Zelenskyy katika hotuba yake ya kila siku usiku.

Ameongeza kwamba  Urusi bado haijasimamisha mashambulizi, ingawa imeshuhudia kupata hasara kubwa katika uwanja wa mapambano.

Soma pia:UN Kupigia kura azimio la uvamizi wa Urusi nchini Ukraine

Aikizungumzia shambulizi la Jumanne dhidi ya Kherson ambalo liliuwa watu wasiopungua 6, amelitaja kuwa ni ujumbe wa dhahiri kwa ulimwengu.

Katika hatua nyingine Rais Zelensky anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa kilele wa NATO utaofanyika Vilnius mwezi Julai.

Amnesty:Wanaohusika na uhalifu Ukraine wakabiliwe na sheria

Katibu Mkuu wa shirika la nchini Ujerumani, Markus Beeko amesema leo Jumatano kwamba, Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha wanaohusika na uhalifu chini ya sheria ya kimataifa, Ukraine wanafikishwa mbele ya sheria.

Amnesty: Urusi imefanya uhalifu Ukraine

01:01

This browser does not support the video element.

Katika tamko lake lililonakiriwa na vyombo vya habari Beeko amesisitiza juu ya kufanyika kwa uchunguzi wa makamanda wa ngazi za juu za kijeshi kadhalika viongozi wa kiraia.

Kwa mujibu wa Amnesty, tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 24, 2022, vikosi vya Moscow vimefanya uhalifu wa kivita na ukiukaji wa sheria za kimataifa za binadamu.

Soma pia:Mashirika ya UN yaomba dola bilioni 5.6 kuwasidia Waukraine

Miongoni mwa ukiukwaji ni pamoja na mauaji ya kinyume na sheria, unyanyasaji wa kingono na kijinsia, mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu, uhamisho wa raia pamoja na mauaji ya kiholela kwa kiwango kikubwa kutokana na kushambulia miji.

Uvamizi iliofanya urusi ni kitengo cha uchokozi kinyume cha sheria ya kimataifa ambao umesababisha janga kubwa la haki za binadamu.

Beeko amesema "waukraine wameishi maisha ya kutisha kaika kipindi cha miezi 12 ya vita".

Katika tamko lake ameongeza kwamba Ukraine inastahili fidia ya kimwili,kiakilikutokana na mateso ya kiuchumi waiosababishwa na rais Vladimir Putin pamoja na vikosi vyake vya Urusi.

"Jumuiya ya kimataifa ina wajibu kuwawajibisha wahusika.” Alisisitiza.